• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Benzema aomba kulitumikia taifa lingine

  (GMT+08:00) 2019-11-18 19:09:23

  Mshambuliaji wa mabingwa wa kihistoria wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid, Karim Benzema ambaye ni raia wa Ufaransa, ameliomba taifa hilo kumruhusu kutafuta taifa lingine la kulitumikia katika soka. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31, ametuma maombi hayo baada ya kuachwa tena kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kwenye michezo ya kufuzu kushiriki Kombe la Euro 2020, ambapo mara mwisho kuitumikia timu ya taifa ilikuwa ni mwaka 2015. Mbali na kuwa kwenye kiwango kizuri, chama cha soka nchini Ufaransa kikaachana na mchezaji huyo kuanzia kwenye michuano ya Euro 2016 kwenye ardhi ya nyumbani pamoja na Kombe la Dunia mwaka jana huku taifa hilo likichukua ubingwa.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako