Mwanzilishi wa Jukwaa hilo, Edrick Mashamba amesisitiza kuwa jukwaa hilo ni ukombozi kwa wakulima na wafanyabiashara wa mazao katika kupata taarifa zitakazopelekea kupunguza au kuondoa kabisa hasara pamoja na urasimu.
Aliongeza kuwa E-Sokoni imedhamiria kuipa thamani sekta ya kilimo kwa kufanya wakulima kujivunia pamoja na kurahisisha maisha ya Mtanzania kupata chakula kwa urahisi na bei rafiki.
Alisema kuwa jukwaa hilo ni fursa kwa maafisa ugani kwani litawasogeza karibu na wateja na kuwaondolea gharama za ziada huku akiomba serikali kupitia Wizara ya Kilimo kuwaunga mkono kuifanya sekta ya kilimo kuwa na manufaa kwa kila mtu anayejihusisha nayo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |