Mwenyekiti wa kampuni ya Isuzu World ambayo ni maarufu kwa uundaji, utengenezaji na ukarabaiti wa magari Eisaku Akazawa amekuwa nchini akitokea Japan ili kumtuza Kipchoge katika hafla iliyoandaliwa katika Msitu wa Karura.
Hii ilikuwa ni baada ya mwanariadha huyo aliyekuwa na mkewe Grace pamoja na watoto wao watatu, kuongoza washiriki wapatao 200 wakiwemo wanafunzi, kukimbia umbali wa kilomita nne hapo Karura.
Oktoba 12, 2019, Kipchoge alitumia muda wa 1:59:41 kukamilisha mbio za "Ineos 1:59 Challenge" jijini Vienna, Austria.
Gari alilotuzwa lina nambari za usajili KCW 159V, ambapo "159V" inaendana na muda wa saa 1:59 na V kuwakilisha jiji la Vienna.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |