• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wahamiaji 21 haramu wafukuzwa kutoka Mashariki mwa Libya kwenda Nigeria

  (GMT+08:00) 2019-11-19 08:25:02

  Mamlaka ya uhamiaji ya Libya mjini Benghazi imetangaza kuwafukuza wahamiaji 21 haramu kwenda Nigeria. Taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo inasema, wahamiaji hao haramu walirudishwa Lagos, Nigeria kwa ndege kutoka uwanja wa kimataifa wa Benina mjini Benghazi.

  Jumapili mamlaka hiyo pia ilitangaza kuwafukuza zaidi ya wahamiaji 60 haramu kutoka Benghazi kwenda Chad na Sudan.

  Shirika la Uhamiaji la Kimataifa IOM limesema Libya ina wahamiaji zaidi ya laki 6.5, elfu sita kati yao wakiwa ni wanawake na watoto, ambao wanashikiliwa kwenye vituo vya mahabusu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako