• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • UM waahidi kuzisaidia kampuni ndogo za Afrika kuingia soko la India

  (GMT+08:00) 2019-11-19 08:25:31

  Kituo cha Biashara cha Kimataifa ITC kimeahidi kuzisaidia kampuni ndogo na zenye ukubwa wa kati za Afrika kuingia kwenye soko la India.

  Mratibu wa mradi wa ITC wa kuunga mkono biashara na uwekezaji wa India kwa Afrika Bw. Govind Venuprased amesema mjini Nairobi kuwa shirika lake linatoa uungaji mkono wa kiushauri na kimkakati kwa kampuni ndogo za Ethiopia, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda ili kuziwezesha kuinua nguvu yao ushindani.

  Akiongea kando ya Jukwaa la biashara ya kilimo kati ya Kenya na India, Bw. Venuprasad amesema kupitia ushirikiano na taasisi na kampuni za India, ITC inaziwezesha kampuni ndogo za Afrika kujihusisha kwenye minyororo ya thamani ya kilimo ili kuongeza mapato yao kupitia kuuza bidhaa zao nje.

  Shirikisho la Mashirika ya Uuzaji Nje ya India FIEO linafanya ziara nchini Kenya, likiwa na ujumbe wenye kampuni 27 kutoka India zinazoshughulika na sekta ya kilimo, ambazo zinatafuta uwekezaji, ubia na fursa nyingine za kibiashara.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako