• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wataalam na watunga sera wakusanyika Ethiopia kujadili mchango wa maeneo maalum ya uchumi kuhimiza maendeleo ya viwanda Afrika

  (GMT+08:00) 2019-11-19 08:38:26

  Viongozi wanaongeza maeneo maalum ya uchumi ya nchi za Afrika SEZs, wataalam na watunga sera wamekusanyika mjini Addis Ababa kujadili mchango wa maeneo hayo kwenye kuhimiza maendeleo ya viwanda barani Afrika.

  Mkutano wa nne wa mwaka wa maeneo ya uchumi ya Afrika unaofanyika kwa siku tatu kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika, unafanyika chini ya kauli mbiu ya maeneo hayo kuhimiza maendeleo ya viwanda barani Afrika. Mkutano huo pia utahusisha siku ya viwanda ya Afrika itakayohudhuriwa na baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika, kujadili changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na sera kuhusu maendeleo ya viwanda Afrika.

  Maeneo maalum ya viwanda barani Afrika yamekuwa maarufu na kutoa mchango mkubwa kwa ongezeko la uchumi na pato kwa nchi za Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako