• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wadau wa utalii wa Kenya wazindua kampeni ya kuhimiza utalii

  (GMT+08:00) 2019-11-19 09:03:08

  Wadau wa utalii wa biashara wa Kenya wamesema kwenye maonyesho ya soko la utalii IBTM huko Barcelona wamezindua kampeni ya kutangaza Kenya kama mahali pa kufanyika shughuli za biashara na mikutano.

  Afisa mkuu mtendaji wa Kituo cha Mkutano wa Kimataifa cha Kenyatta (KICC) Bibi Nana Gecaga amesema, Kenya ni miongoni mwa washiriki 15,000 wa utalii wa mikutano walioshiriki kwenye maonesho ya IBTM mjini Barcelona, ambayo ni hafla kubwa ya kimataifa kwa sekta ya mikutano na shughuli za biashara.

  Bibi Gecaga amesema Kenya inabadilika kuwa mahali pa utalii wa mikutano barani Afrika, na KICC itaendelea kufanya ushirikiano na mashirika binafsi ili kuifanya Kenya iwe mahali pa shughuli za biashara na mikutano.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako