• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Pompeo asema Marekani haitachukulia ujenzi wa makazi wa Israel katika Ukingo wa Magharibi kukiuka sheria ya kimataifa

  (GMT+08:00) 2019-11-19 09:33:50

  Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo amesema serikali ya nchi hiyo haitauchukulia ujenzi wa makazi wa Israel katika Ukingo wa Magharibi kama ukiukaji wa sheria ya kimataifa, jambo ambalo litaweza kuongeza mvutano kwa hatma ya mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina. Bw. Pompeo amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari kuwa uamuzi huo ambao ni kinyume na msimamo wa serikali ya Marekani iliyoongozwa na Obama imefanywa kwa mujibu wa hali halisi. Msemaji wa ikulu ya Palestina Bw. Nabil Abu Rudeineh amekosoa uamuzi huo na kusema serikali ya Marekani haina mamlaka ya kuhalalisha makazi ya Israel.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako