Mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Microsoft Bill Gates amesema China imepata maendeleo makubwa katika kuinua usawa wa afya na kupunguza umaskini, jambo ambalo linatoa uzoefu ili kusaidia nchi nyingine zinazoendelea haswa zile za Afrika kuongeza maendeleo yao. Kabla ya kuanza ziara ya siku mbili nchini China, Bill Gates ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa Mfuko wa Bill & Melinda uliofungua ofisi yake nchini China mwaka 2007, amesema China imepata mafanikio ya kuvutia katika sekta mbalimbali, kutoka uzalishaji mkubwa wa kilimo, kuinua hali ya afya hadi mfumo wa kielimu wenye nguvu kwa kuwa na vyuo vikuu bora zaidi duniani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |