• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Mataifa wahimiza kupunguza matumizi ya dawa za kuulia wadudu barani Afrika

  (GMT+08:00) 2019-11-19 09:39:08

  Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limeahidi kuunga mkono kuimarisha usimamizi wa matumizi ya dawa za kuulia wadudu katika sekta ya kilimo barani Afrika.

  Ofisa mwandamizi wa ofisi ya FAO barani Afrika anayeshughulikia afya ya wanyama na uzalishaji wa mifugo Bw. Scott Newman, amesema uungaji mkono huo unalenga kupunguza hali ya matumizi mabaya ya dawa hizo katika sekta za kilimo na mazingira, kunakosababisha kutokea na kuenea kwa wadudu wanaoweza kuhimili dawa hizo, na kuleta tishio kubwa kwa kila mtu, na kutishia afya ya kijamii, uzalishaji wa chakula, uanuwai wa viumbe na mazingira ya asili.

  Takwimu zilizotolewa na Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa, matumizi ya dawa za kuulia wadudu yanasababisha vifo vya watu laki saba kila mwaka, na kama yasipodhibitiwa idadi hii itaongezeka kuwa milioni moja hadi kufikia mwaka 2050.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako