• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Korea Kaskazini yakataa kufanya mazungumzo na Marekani juu ya kutokuwepo kwa silaha za nyuklia

    (GMT+08:00) 2019-11-19 16:56:26

    Mkuu wa kamati ya amani ya Asia na Pasifiki ya Korea Kaskazini Bw. Kim Yong-chol jana amesema, nchi hiyo haitafanya mazungumzo na Marekani juu ya suala la kutokuwepo kwa silaha za nyuklia mpaka Marekani itakapofuta msimamo wake mbaya dhidi ya Korea Kaskazini.

    Kauli hiyo imekuja baada ya waziri wa ulinzi wa Marekani Bw. Mark Esper kuamua kuahirisha mazoezi ya anga ya pamoja na Korea Kusini Jumapili iliyopita, na kuilazimisha Korea Kaskazini kufanya mazungumzo tena na Marekani bila sharti lolote.

    Kim Yong-chol amesema, mazungumzo hayo juu ya suala la kutokuwepo kwa silaha za nyuklia yatafanyika kwategemea uaminifu kati ya Korea Kaskazini na Marekani, pamoja na kuondoa matishio mbalimbali dhidi ya usalama na maendeleo ya nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako