• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Aussems – Siogopi kufukuzwa Simba SC

  (GMT+08:00) 2019-11-19 17:15:41
  Kocha wa klabu ya Simba Aussems amesema hana presha wala hofu baada ya fununu za kuitaka kutimuliwa kweny klabu hiyo kumfikia. Amesema kila kitu kinachoendelea juu yake anakijua, ila hana wasiwasi kwa kuwa anatimiza majukumu yake kama kocha wa timu hiyo vyema, na kusema anakiamini kikosi chake. Amesema ni lazima kukutana na changamoto sehemu yoyote unayofanya kazi, na kocha anaajiriwa ili afukuzwe, hivyo hana hofu na anaendelea na majukumu yake. Kocha huyo ameondoka nchini Tanzania juzi alfajiri, na kuwashtua viongozi wa klabu hiyo kwa kuwaaga akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako