• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • RAGA: Kabras, KCB na Homeboyz wanyimana pumzi Kenya Cup

  (GMT+08:00) 2019-11-19 17:20:02

  Timu za Kabras Sugar, KCB na Homeboyz zimebaki katika nafasi tatu za kwanza kwenye Ligi Kuu ya raga nchini Kenya (Kenya Cup) baada ya kila timu kupata ushindi wa nne mfululizo wikendi iliyopita. Mabingwa wa mwaka 2016 Kabras bado wanaongoza ligi hii ya klabu 12 kwa tofauti ya ukubwa wa ushindi wa mechi zao. Wanasukari hao kutoka Kaunti ya Kakamega wana jumla ya alama 20 baada ya kuwafunga Nondescripts 40-15 uwanjani Jamhuri jijini Nairobi. Wamevuna alama sawa na mabingwa watetezi KCB, ambao pia wamefikisha alama 20 baada ya kujiongezea alama ya bonasi ya tano mfululizo kwa kuwafunga Menengai Oilers 43-13 katika uwanja wa kilimo wa Nakuru. Homeboyz ndio timu ya mwisho ambayo haijapoteza mechi. Inashikilia nafasi ya tatu kwa alama 18. Imezoa alama mbili za bonasi. Wanabenki wa KCB wataalika Homeboyz uwanjani Ruaraka katika mechi yao ijayo mnamo Novemba 23.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako