• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Hongkong yatoa wito kwa watu wa ngazi mbalimbali mkoani humo kuacha kuunga mkono wahalifu wanaofanya vurugu

  (GMT+08:00) 2019-11-19 18:38:59

  Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje Bw. Geng Shuang amesisitiza kuwa China inaitaka Marekani kuheshimu mamlaka ya China, na kuacha kutoa kauli zisizo mwafaka, kusimamisha vitendo vya kuvumilia uhalifu na matumizi ya mabavu, na kutoingilia mambo ya Hongkong pamoja na mambo ya ndani ya China. Geng amesema hayo baada ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo hivi karibuni kutoa kauli zisizofaa juu ya hali ya Hong Kong. Aidha mkurugenzi wa Idara ya mambo ya kisiasa ya serikali ya Mkoa wa utawala maalumu wa Hongkong Bw. Zhang Jianzong ametoa wito kwa watu wa ngazi mbalimbali kutounga mkono vitendo vya kufanya vuruga, ili kurejesha mapema utulivu mkoani humo…………

  Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesisitiza kuwa, serikali kuu ya China itaendelea kumuunga mkono kithabiti ofisa mkuu wa mkoa wa Hongkong kuiongoza serikali ya mkoa huo kutekeleza majukumu kwa kufuata sheria, kuunga mkono kithabiti polisi wa Hongkong kutekeleza sheria, na kuunga mkono kithabiti mamlaka ya sheria ya Hongkong kuwaadhibu wahalifu wanaotumia mabavu kwa kufuata sheria. Amesema mambo ya Hongkong ni mambo ya ndani ya China, serikali, mashirika au mtu yeyote hana haki ya kuingilia.

  "Hivi karibuni Marekani imetoa kauli mara kwa mara kuhusu suala la Hongkong, ambayo imeonesha makusudi yao ya kuingilia suala la hilo na vigezo viwili kuhusu uhalifu wa kutumia mabavu."

  Bw. Geng pia ameeleza kuwa baada Hongkong kurudi China mwaka 1997, utekelezaji wa haki na wajibu vinavyohusiana na Uingereza ambazo ziliwekwa kwenye Taarifa ya Pamoja ya China na Uingereza umemalizika. Marekani haina misingi yoyote ya kisheria wala haki ya kutoa lawama yoyote kuhusu mambo ya Hongkong kwa kunukuu taarifa hiyo. Bw. Geng Shuang anasema:

  "Nasisitiza kwa mara nyingine tena, serikali ya China inashikilia nia thabiti katika kulinda mamlaka na usalama wa nchi, maslahi ya kujiendeleza, kutekeleza mwongozo wa 'nchi moja na mifumo miwili', na kupinga nguvu za nje kuingilia mambo ya ndani ya Hongkong."

  Kutokana na vyuo vikuu vingi vya Hongkong kuathiriwa vibaya katika siku kadhaa zilizopita, mkurugenzi mkuu wa Idara ya mambo ya kisiasa ya serikali ya mkoa wa utawala maalumu wa Hongkong Bw. Zhang Jianzong anasema:

  "Vitendo vya kimabavu vilivyotokea kwenya Chuo Kikuu cha Polytechnic vimefikia kiwango cha kuchochea vurugu, watu wanaobaki au kuwasaidia wahalifu wanaotumia mabavu wanaweza kuhukumiwa kwa kuchochea vurugu. Nawataka watu wanaobaki kwenye chuo hicho kufuata maelekezo ya polisi na kuondoka kutoka chuo hicho. Serikali ya mkoa wa Hongkong inasikitishwa kwa kuharibiwa vibaya kwa vyuo vikuu vingi mkoani humo. Tunawataka watu wajizuie na kudumisha utulivu, kuacha kuunga mkono uhalifu wa kutumia mabavu, ili kurejesha utulivu mkoani Hongkong mapema."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako