• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalam wazitaka serikali za Afrika kutoa kipaumbele kwa uzazi wa mpango ili kupunguza migogoro

    (GMT+08:00) 2019-11-19 18:44:23

    Serikali za nchi za Afrika zinatakiwa kutoa kipaumbele katika uzazi wa mpango ili kusaidia kupunguza migogoro ya kisiasa.

    Wito huo umetolewa na wataalamu kando ya mkutano wa 8 wa Idadi ya watu barani Afrika (APC) unaofanyika Entebbe, nchini Uganda. Wamesema kasi kubwa ya ongezeko la idadi ya watu pamoja na kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira ni sehemu ya sababu za migogoro ya kisiasa, ambayo inasababisha kuvuruga mipango ya maendeleo.

    Katika mkutano huo wa siku nne ulioanza jana, wanasayansi wa Afrika wanajadili njia za kutumia vizuri ongezeko la watu kwa ajili ya maendeleo endelevu.

    Mkutano huo unafanyika kila baada ya miaka minne, na mara ya mwisho ulifanyika Pretoria, Afrika Kusini mwaka 2015.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako