• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Rwanda yasaka watalii Dubai

    (GMT+08:00) 2019-11-19 19:32:24
    Wadau wa sekta binafsi na serikali kutoka Rwanda wako katika milki za kiarabu kutafuta wawekezaji kwenye mkutano wa Biashara wa Afrika wa mwaak 2019.

    Mkutano huo umeandaliwa na chama cha Biashara na Viwanda cha Dubai chini ya maudhui ya 'Kuongeza ukuaji Afrika' na unahudhuriwa na Wakuu wa Nchi, mawaziri, watunga sera, viongozi mashuhuri wa biashara, wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Afrika na kwingineko.

    Rwanda inawalenga wawekezaji ambao wapo katika soko la UAE na wanatafuta nafasi za kuwekeza Afrika na pia wale ambao wanawekeza kupitia Dubai kutokana na miundombinu yake ya uwekezaji.

    Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Maendeleo ya Rwanda, Clare Akamanzi ambaye alifanya mikutano kadhaa na wawekezaji amesema wanalenga wawekezaji wa sekta kadhaa kama vile madini, usindikaji wa bidhaa za kilimo, na utalii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako