• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Zanzibar yashauriwa kuhusu mikataba ya mafuta 

  (GMT+08:00) 2019-11-19 19:33:22
  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imeshauriwa kuwa makini inapoingia makubaliano ya kibiashara ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia kwa lengo la kunusuru athari za kimazingira hasa kipindi cha uzalishaji.

  Akiwasilisha mada ya mgawanyo wa mapato ya mafuta katika mafunzo kuhusu mafuta na gesi asilia kwa wanasheria wa serikali, Mshauri Mwelekezi wa Mafuta na Gesi, Yona Killagane, alisema uchimbaji wa mafuta unatumia fedha nyingi, hivyo bila kuwa na uamuzi wenye maslahi ya taifa, unaweza kusababisha serikali kuingia hasara.

  Killagana alisema nchi nyingi zinazoendelea zinaingia hasara kwa kukosa sera makini, hivyo kuwataka kufahamu majukumu yao katika kuhakikisha wanakuwa na mipango imara ya kulinda sekta hiyo.

  Pia aliishauri Mamlaka ya Udhibiti na Utafutaji Mafuta na Gesi Asilia (ZPDC) kuhakikisha watakapopata mikataba ya kutafuta na kuchimba mafuta, isiingie katika mfumo wa kukodi majengo au vifaa kwa kuwa watakapomaliza watashindwa kunufaika na gharama zinazoweza kutumiwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako