• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wizara ya biashara ya Marekani yaahirisha kwa mara ya tatu baadhi ya marufuku dhidi ya biashara za kampuni ya Huawei ya China

  (GMT+08:00) 2019-11-19 20:16:26

  Wizara ya biashara ya Marekani imeamua kuongeza kibali cha muda kwa siku 90, ikiwa ni mara ya tatu kuongeza muda wa kuzuia bidhaa na huduma za kampuni ya Huawei ya China Huawei na kampuni zake tanzu nchini Marekani, ili kuepusha athari mbaya zinazotokana na hatua hiyo kwa wateja wake nchini humo.

  Taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo imesema, kampuni za Marekani zilizopata kibali hicho zinaweza kuuza na kuhamisha bidhaa na teknolojia maalumu kwa kampuni ya Huawei na kampuni zake tanzu katika siku 90 zijazo.

  Mei 15, wizara hiyo iliiweka Huawei na kampuni zake tanzu 68 kwenye orodha nyeusi. Lakini Mei 20 na Agosti 19 ilitoa kibali cha muda cha siku 90, ambacho kinairuhusu kampuni ya Huawei na kampuni zake tanzu kufanya shughuli maalumu, ili kuhakikisha uendeshaji wa mtandao husika wa Marekani na kuunga mkono huduma husika za simu za mkononi za nchi hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako