• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • UNICEF yasema watoto maskini zaidi hawajafaidika katika miaka 30 iliyopita tangu Mkataba wa Haki za Watoto kupitishwa

  (GMT+08:00) 2019-11-19 20:16:41

  Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa limetoa ripoti ikisema, katika miaka 30 iliyopita tangu Mkataba wa Haki za Watoto kupitishwa, huduma kwa watoto kote duniani zimeboreshwa, lakini watoto wengi maskini au wenye hali duni wamepata faida ndogo.

  Ripoti hiyo imesema, kiwango cha vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kote duniani kimepungua kwa asilimia 60 katika miaka 30 iliyopita, na kiwango cha ukosefu wa elimu kwa watoto kimepungua kutoka asilimia 18 hadi 8. Lakini ripoti hiyo pia imesema, hivi sasa maendeleo yaliyopatikana yamekosa uwiano. Katika nchi zenye pato la katikati na chini, kiwango cha watoto wanaofariki kutokana na maradhi yanayoweza kuzuilika katika familia maskini ni maradufu ikilinganishwa na kiwango hicho katika familia tajiri.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako