• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yalaani Marekani kupitisha mswada wa haki za binadamu na demokrasia kuhusu Hong Kong

  (GMT+08:00) 2019-11-20 10:22:31

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang ametoa kauli kuhusu baraza la seneti la bunge la Marekani kupitisha mswada wa haki za binadamu na demokrasia kuhusu Hong Kong, akilaani kuwa mswada huo umepotosha ukweli, kutumia vigezo tofauti, kuingilia mambo ya ndani ya China na kukiuka kanuni za sheria na uhusiano wa kimataifa.

  Bw. Geng amesema katika miezi mitano iliyopita, vitendo vya kimabavu vilivyotokea mkoani Hong Kong vimetishia usalama wa maisha na mali ya umma, kukiuka sheria na utaratibu wa kijamii, kuharibu ustawi na utulivu wa mkoani huo, na kutishia kanuni ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili". Ameongeza kuwa hivi sasa suala kuu linaloikabili Hong Kong si haki za binadamu na demokrasia, bali ni kumaliza vurugu, kulinda sheria na kurejesha utaratibu.

  Ofisi ya mambo ya Hong Kong na Macao ya baraza la serikali la China, ofisi ya mawasiliano ya serikali kuu ya China mkoani Hong Kong, na kamati ya mambo ya nje ya Baraza la Kudumu la Bunge la Umma la China pia zimelaani mswada huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako