• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matokeo mapya ya sayansi na teknolojia za reli yaliyopatikana ndani na nje ya China yaoneshwa mjini Beijing

  (GMT+08:00) 2019-11-20 18:09:21

  Maonesho ya 15 ya kimataifa ya China ya teknolojia na vifaa za kisasa vya reli yamefanyika leo mjini Beijing, na kuonesha maendeleo na matokeo mapya kuhusu sayansi na teknolojia za reli zilizopatikana ndani na nje ya nchi. Reli ya mwendo kasi ya Fu Xing, na Reli ya mwendo kasi ya Jing Zhang inayotumia teknolojia ya akili bandia zimeoneshwa na kuwa kivutio kikubwa kwenye maonesho hayo.

  Kwenye maonesho hayo, roboti inayotoa huduma kwa abiria kwa kutumia akili bandia ambayo ilitengenezwa na Kampuni ya Chuo cha utafiti wa sayansi cha reli cha China inawavutia watu wengi. Mfanyakazi Zhang Yatao ameeleza kuwa, roboti hiyo inatarajiwa kutumiwa katika reli ya mwendo kasi ya Jing Zhang ambayo inatazamiwa kuanza kazi rasmi hivi karibuni, na kutoa huduma za kufanya utafutaji wa habari, kuelekeza usafiri na kuchukua mizigo.

  "Unaweza kupata uhakika kuhusu tiketi, kituo cha kuondoka au kufika kwa treni, mlango wa ukaguzi wa tiketi, ama kupata maelekezo ya kwenda msalani au maduka, kupitia roboti hii inayoweza kusoma kadi ya kitambulisho, nambari za QR na kutambua sura za watu."

  Maonesho hayo yanahusisha sekta mbalibali zikiwemo ujenzi wa mtandao wa barabara, uchukuzi wa abiria na mizigo, mambo ya uendeshaji na usimamizi, ujenzi wa miradi, mitambo ya teknolojia na utoaji wa huduma kwa abiria. Kampuni mbalimbali zinazohusika kutoka nchi za nje ikiwemo Siemens, Bombardier, Knorr-Bremse na Westinghouse zimeshiriki katika maonyesho hayo. Ofisa wa Kampuni ya Siemens anayeshughulikia mambo ya China Zhan Qianhui anasema:

  "Kujenga barabara zinazounganishwa ni kazi kuu kwa sasa, na lengo la siku za baadaye la Kampuni ya Siemens. Kupitia Sand table model, unaweza kuona mipango yetu ya kuunganisha barabara kuu, barabara kati ya miji mbalimbali na ndani ya miji, pamoja na maendeleo yaliyopatikana katika sekta ya uvumbuzi wa kidijitali."

  Meneja mkuu wa Kundi la Reli la China Bw. Yang Yudong ameeleza kuwa, kuendeleza reli inayotumia akili bandia kutakuwa mkakati muhimu wa kampuni hiyo wa kufanya uvumbuzi wa sayansi na teknolojia za reli katika siku zijazo.

  "Tutahimiza kwa nguvu utatuzi wa teknolojia muhimu katika vifaa vya akili bandia, kuzidi kuboresha vigezo vinavyohusika kwenye reli ya mwendo kasi, ili kutengeneza reli mpya za mwendo kasi zilizo na usalama zaidi, safi zaidi na kubana nishati kwa wingi zaidi."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako