• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Algeria wamkataa Karim Benzema

    (GMT+08:00) 2019-11-20 18:16:23
    Kocha wa timu ya taifa Algeria, Djamel Belmadi, amesema wachezaji alionao wa timu hiyo wanatosha, hivyo hana mpango wa kumpa nafasi nyota wa timu ya taifa ya Ufaransa, Karim Benzema. Benzema ambaye alikuwa mchezaji wa timu ya taifa Ufaransa, ameachwa kwenye kikosi hicho tangu mwaka 2015 kutokana na kashfa ya kumiliki mkanda wa ngono wa mchezaji mwenzake, hivyo shirikisho la soka nchini humo likaamua kuachana na mchezaji huyo kutokana na tukio hilo. Mwishoni mwa wiki iliopita mchezaji huyo alitumia ukurasa wake wa Twitter kumuomba rais wa shirikisho hilo kumruhusu atafute taifa lingine kwa ajili ya kulitumikia kwenye soka kwa kuwa wao hawana mpango naye.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako