• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa IGAD azitaka pande zinazopingana nchini Sudan Kusini kutimiza majukumu yaliyowekwa kabla ya muda wa mwisho kufika

    (GMT+08:00) 2019-11-20 19:06:46

    Shirika la Maendeleo la Kiserikali la Nchi za Afrika Mashariki IGAD limezitaka pande zinazopingana nchini Sudan Kusini kumaliza tofauti zilizopo kabla ya muda wa mwisho wa siku 100 uliowekwa kufika.

    Wito huo umetolewa na mjumbe maalum wa IGAD nchini Sudan Kusini Ismail Wais, alipoongoza kongamano la siku mbili lililoandaliwa na IGAD kwa mfumo wa usalama.

    Amesema muda wa siku 100 unatoa fursa nyingine ya kupanga na kutekeleza kazi zilizosalia, na kuwataka kutimiza kazi hiyo ndani ya siku 60, ili kuepuka hatari yoyote ya kutokamilisha majukumu hayo kabla ya wakati kutokana na mapumziko na sikukuu za mwisho wa mwaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako