• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China akutana na mkuu wa Benki ya Dunia

    (GMT+08:00) 2019-11-21 09:08:15

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amekutana na mkuu wa Benki ya Dunia (WB) Bw. David Malpass na kuonesha nia ya kupenda kuimarisha ushirikiano kati yao katika sekta muhimu.

    Bw. Li amesema China inazingatia kuendeleza uhusiano na Benki ya Dunia ambayo ni shirika la maendeleo la pande nyingi, na iko tayari kuongeza ushirikiano na benki ya dunia katika sekta za uhifadhi wa mazingira, uanuai wa viumbe na kuondoa umaskini kupitia ushirikiano wa kifedha na kiakili. Pia China itatekeleza majukumu yake ya kimataifa ya nchi kubwa inayoendelea ili kuhimiza maendeleo ya kimataifa.

    Bw. Malpass amesema maendeleo ya uchumi wa China yana mustakbali mzuri, na mafanikio makubwa yamepatikana katika kufungua mlango kwa nje. Benki ya dunia inapenda kuimarisha ushirikiano na China katika nyanja za ukuaji wa uchumi, kuzeeka kwa watu, uvumbuzi wa sayansi na teknolojia na uhifadhi wa mazingira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako