• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNAMID yatoa wito pande mbalimbali za Sudan zishiriki mchakato wa amani

    (GMT+08:00) 2019-11-21 09:08:49
    Mjumbe maalum wa Tume ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika katika Darfur (UNAMID) Bw. Jeremiah Mamabolo ametoa wito kwa pande mbalimbali za Sudan kushiriki kwenye mchakato wa amani.

    Bw. Mamabolo ameihimiza serikali ya Sudan na makundi mbalimbali nchini humo, kushirikiana na Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa kuwaruhusu na kuwaunga mkono wafanyakazi wa misaada kufika kwenye maeneo ya mbali ikiwemo Darfur, ili kuhakikisha misaada ya kibinadamu inatolewa kwa wakati na kwa ufanisi..

    Bw. Mamabolo pia amesema UNAMID itaendelea kuunga mkono mchakato wa amani kati ya serikali ya Sudan na makundi mbalimbali ya Darfur.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako