• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yailalamikia Marekani kwa kupitisha mswada kuhusu Hong Kong

  (GMT+08:00) 2019-11-21 09:46:52

  Naibu waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Ma Zhaoxu amekutana na kaimu balozi wa Marekani nchini China Bw. William Klein, akipinga vikali baraza la seneti la bunge la Marekani kupitisha "msawada wa haki za binadamu na demokrasia kuhusu Hong Kong". Bw. Ma amesema Hong Kong ni sehemu ya China, na mambo yake ni mambo ya ndani ya China, ambayo hayaruhusiwi kuingiliwa na nchi nyingine, na mswada huo umeingilia mambo ya ndani ya China, na kukiuka kanuni ya sheria na uhusiano wa kimataifa. Ameionya Marekani kuwa hila yoyote ya kuzuia maendeleo ya China haitafanikiwa, na badala yake itajidhuru yenyewe.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako