• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kongamano la uchumi wa uvumbuzi lafunguliwa Beijing

  (GMT+08:00) 2019-11-21 15:57:47

  Kongamano la uchumi wa uvumbuzi limefunguliwa leo mjini Beijing, ambapo makamu wa rais wa China Bw. Wang Qishan amehudhuria na kuhutubia ufunguzi huo.

  Kongamalo hilo limeshirikisha maofisa wa serikali, viongozi wa zamani wa kisiasa na mabingwa wa biashara zaidi ya 600 kutoka nchi na sehemu zaidi ya 60 duniani. Washiriki hao watajadili juu ya sekta mbalimbali ikiwemo usimamizi wa mfumo wa uchumi wa dunia, biashara, sayansi na teknolojia, na masoko ya mitaji, na mkakati wa kukabiliana na changamoto kuu zinazoikabili dunia nzima.

  Kwenye hotuba yake, Bw. Wang Qishan amesisitiza kuwa China itafuata njia ya kujiendeleza kwa amani, na kushirikiana na watu wote katika kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, kukabiliana na changamoto kuu za dunia, kuhimiza amani na maendeleo ya dunia, na kutafuta ufumbuzi mpya juu ya masuala ya utaratibu wa usimamizi wa dunia, uaminifu, amani na maendeleo. Ameongeza kuwa nchi zote zinapaswa kulinda mfumo wa kimataifa ambao kiini chake ni Umoja wa Mataifa, kujenga mfumo mpya wa utatuzi wa migogoro duniani wenye haki na usawa, na kuwafanya watu wote duniani wanufaike pamoja na maendeleo ya mafungamano ya kiuchumi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako