• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China Bara na Hongkong zasaini marekebisho ya makubaliano kuhusu biashara ya utoaji wa huduma

    (GMT+08:00) 2019-11-21 18:36:29

    Naibu waziri wa biashara wa China Bw. Wang Bingnan na mkurugenzi wa Idara ya fedha ya Hongkong Bw. Chen Maobo wamesaini makubaliano yaliyorekebishwa ya biashara ya utoaji wa huduma ya "Mipango kuhusu kuanzisha uhusiano wa karibu zaidi wa kiuchumi na kibiashara kati ya China Bara na Hongkong", yatakayoanza kutekelezwa Juni 1, mwaka kesho…

    Bw. Wang Bingnan ameeleza kuwa, makubaliano hayo yanahusisha hatua mpya za ufunguaji mlango katika sekta ya biashara ya utoaji wa huduma baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya awali mwaka 2015. Makubaliano hayo yanaondoa au kupunguza masharti ya kuidhinisha watoaji wa huduma katika sekta mbalimbali za fedha na sheria kwa mujibu wa matakwa ya sekta zinazohusika za Hongkong, na kupanua maeneo ya kukubaliana kwa sifa za wataalamu wanaohusika, ili kuweka mazingira mazuri kwa waHongkong kuanzisha biashara China Bara.

    Bw. Wang Bingnan amesisitiza kuwa, serikali kuu inaunga mkono kithabiti serikali ya mkoa wa utawala maalumu wa Hongkong, na kuamini kuwa Hongkong hakika itaondokana na matatizo yanayoikabili hivi sasa.

    "Serikali kuu ni muungaji mkono thabiti wa Hongkong, si kama tu itaisaidia Hongkong kukabiliana na matishio, na kushinda changamoto mbalimbali, bali pia itatoa fursa kubwa kwa Hongkong katika kutafuta njia mpya ya kujiendeleza."

    Bw. Chen Maobo ameeleza kuwa, makubaliano yaliyorekebishwa yameongeza hatua za kufungua mlango katika sekta nyingi za utoaji wa huduma, ikiwa ni pamoja na fedha, sheria, televisheni na filamu, na utoaji wa huduma za utalii ambazo zinaongozwa na Hongkong.

    Pia ameeleza kuwa, kufufuka kwa utaratibu wa kujilinda kibiashara na vitendo vya upande mmoja kumedhuru biashara ya kimataifa, na pia kukwamisha maendeleo ya uchumi wa dunia. Makubaliano hayo yaliyorekebishwa yameonesha nia imara ya China Bara na Hongkong katika kuhimiza ufunguaji mlango wa soko na biashara huria. Pia amesema hivi sasa China Bara ni soko kubwa zaidi la matumizi ambayo inatoa fursa nyingi. Bw. Chen Maonan anasema:

    "Ili kuyasaidia makampuni ya Hongkong kutumia vizuri fursa hizo za biashara, Serikali ya mkoa wa Hongkong imetangaza kuingiza fedha katika mfuko maalumu unaolenga kuongeza ushawishi wa chapa, kupandisha ngazi ya uzalishaji na kupanua soko la mauzo ya bidhaa, na kuongeza msaada wa fedha kwa kila kampuni ya Hongkong inayoanzisha biashara China Bara hadi kufikia dola za kimarekani laki 2.5."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako