• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wataka hatua za haraka zichukuliwe kukabiliana na hali mbaya ya usalama katika kanda ya Sahel

    (GMT+08:00) 2019-11-21 18:39:59

    Msaidizi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Afrika Bi. Bintou Keita ameliambia Baraza la Usalama la Umoja huo kuwa hali ya usalama katika eneo la Sahel barani Afrika imeendelea kuzorota kutokana na kuongezeka kwa mashambulizi ya kigaidi.

    Amesema katika miezi sita iliyopita, usalama katika eneo hilo umekuwa wa wasiwasi mkubwa na hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa, na kwamba kuongezeka kwa mashambulizi dhidi ya vikosi vya usalama na raia na uchonganishi kati ya jamii moja na nyingine vinavyofanywa na makundi yenye silaha kunaongeza kuzorota kwa usalama katika eneo hilo.

    Bi. Keita amesema, katika miezi sita iliyopita, Burkina Faso, Mali na Niger zimekumbwa na mashambulizi mabaya zaidi dhidi ya majeshi ya nchi hizo, na kuongeza kuwa vurugu zinazosababishwa na ugaidi zimeenea mpaka kwenye ukanda wa Sahel na Sahara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako