Katika Mkutano wa Bodi ya Usimamizi jana,Mkurugenzi Mtendaji wa UN-Habitat Maimuna Shariff alisema Shirika hilo kwa sasa halina fedha za kutekeleza miradi yake.
Aidha alisema tangu achukue uongozi wa Shirika hilo mapema mwaka jana,alipata shirika hilo likipitia changamoto za kifedha na hivyo kusitisha shughuli za kuwaajiri watu upya.Alisema kufikia sasa kuna nafasi za kazi 34 ambazo hazijajazwa kutokana na uhaba wa fedha.
Bi Shariff aliyapongeza mataifa ya Kenya na Norwaykwa kuongezea mchango wao kila mwaka.
Kenya imeongeza mchango wake kutoka Sh70 milioni hadi Sh100 milioni.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |