• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Tanzania kuanzisha wakala wa kilimo cha maua, mboga na matunda

    (GMT+08:00) 2019-11-21 19:42:11
    Mchakato wa serikali ya Tanzania wa kuanzisha Wakala wa Maendeleo ya Kilimo cha Maua,Mboga na Matunda ili kuchochea mkakati mpya wa kufikia mapinduzi ya kijani umeiva.

    Jana,Naibu Waziri wa Kilimo,Hussein Bashe,alisema wakala huyo atajulikana kama "Horticulture Develpoment Agency" (HAD).

    Kwa mujibu wa Bashe,mchakato huo utakuwa umekamilika rasmi ifikapo Februari mwaka 2020,ukilenga zaidi kuchochea ukaji wa sekta ndogo ya kilimo hicho.

    Alisema wakala wa Maendeleo ya Kilimo cha Maua,Mboga na Matunda atasaidia kuondoa vikwazo vyote vinavyokwaza sekta hiyo ndogo,lakini yenye manufaa makubwa,na kuchochea ukuaji wake kwa kasi.

    Bashe alidokeza kuhusu mchakato huo baada ya kukutana na wadau wa sekta hiyo wakiongozwa na Taasisi Kilele ya Kilimo hicho yaani Tanzania Horticulutural Association.

    Chombo hicho kinachotarajiwa kuibeba sekta hiyo,kinatarajiwa kuchangia kwenye uchumi wa taifa kiasi cha dola za marekani bilioni 1.85 kwa mwaka ifikapo mwkaa 2021.

    Mchango huo wa sekta ya matunda na mboga utakuwa umepanda kutoka dola milioni 764 za marekani inayochangia kwa sasa na kuajiri vijana na wanawake kwa wingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako