• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda-Makampuni ya ndani yataka ulinzi kutokana na bidhaa zinazoagizwa kutoka nje

  (GMT+08:00) 2019-11-21 19:42:34
  Wenye viwanda wa ndani nchini Rwanda wanadai kuwa uagizaji wa bidhaa shindani,gharama za juu za umeme na uagizaji mali ghafi na uendeshaji wa chini unatatiza ushindani wao katika masoko ya ndani na kimataifa.

  Changamoto hizo zilitajwa jana wakati wa maadhimisho ya Siku ya Viwanda Afrika.

  Siku hiyo inatoa fursa ya kubadilishana mafanikio,uzoefu,chanagmoto na matarajio ya maendeleo ya siku zijazo katika sekta ya viwanda Rwanda.

  Siku hiyo iliadhimishwa chini ya kaulimbiu : "Kukiweka kiwanda cha Afrika kiweze kuhudumia Eneo la Soko Huru Barani Afrika (AfCFTA).

  Meneja Mauzo katika kiwanda cha chuma cha Master Steel,Constantin Rugaba, alisema bidhaa shindani zinazoagizwa kutoka nje zimefanya mauzo yao kupungua.

  Alisema wanazalisha mabati,misumari,vyuma,na bidhaa nyingine muhimu za ujenzi.Hata hivyo wanakabiliwa na changamoto ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje ambazo wakati mwingine hazifikii viwango na kuuzwa kwa bei rahisi kuliko bidhaa zao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako