• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Kina dada wa Harambee Starlets waitambia Crested Cranes ya Uganda kwa 3-0 michuano ya Cecafa

  (GMT+08:00) 2019-11-22 08:56:14

  Kinadada wa Harambee Starlets wamekamilisha mechi zao za Kundi B bila kushindwa baada ya kuwalipua wenzao wa Crested Cranes ya Uganda 3-0 kwenye mashindano ya soka ya wanawake ya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) uwanjani Chamazi jijini Dar es Salaam, Tanzania, jana Alhamisi. Starlets inayofundwa na kocha David Ouma, ambayo iliibamiza Ethiopia 2-0 Novemba 17 na kuibebesha Djibouti kapu la magoli 12-0 Novemba 19 katika mechi mbili za kwanza, iliinyamazisha Uganda kupitia mabao ya Mercy Airo na Mwanahalima Adam Jereko. Kenya imemaliza ikiwa kinara wa kundi lake kwa alama tisa ikifuatiwa na Uganda (sita) nayo Ethiopia imejiondolea aibu ya kubanduliwa nje mapema baada ya Djibouti 8-0. Starlets italimana na Burundi nayo Uganda itavaana na Tanzania katika mechi za nusu-fainali kesho Novemba 23. Tanzania pia ilishinda mechi zake zote za Kundi A dhidi ya Sudan Kusini (9-0), Burundi (4-0) na Zanzibar (7-0). Burundi ilimaliza ya pili katika kundi hilo baada ya kuipepeta Zanzibar 5-0 na Sudan Kusini 3-0. Sudan Kusini ilizoa ushindi mmoja ilipoishangaza Zanzibar kwa 5-0. Fainali ni Novemba 25.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako