• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • WALEMAVU: NPC-Rwanda yatishia kulishitaki shirikisho la Mpira wa wavu wa walemavu la Kenya

  (GMT+08:00) 2019-11-22 08:56:31

  Kamati ya Taifa ya Wachezaji Walemavu nchini Rwanda (NPC-Rwanda) imetishia kulishitaki shirikisho la Mpira wa wavu wa walemavu la Kenya kwa kutotoa malipo kwenye michuano ya mabingwa wa Mpira wa wavu wa walemavu yaliyofanyika Kigali mwezi Septemba. Kauli hiyo ameitoa rais wa zamani wa NPC Celestin Nzeyimana, ambaye alikuwa mkuu wa kamati ya maandalizi ya mashindano. Deni hilo la kiasi cha $26,250 linatokana na kutolipa ada ya ushiriki na huduma za hoteli. Timu za wanawake na wanaume za Kenya zilikuwa na jumla ya watu 35. Michuano hiyo pia ilikuwa ni ya kufuzu michezo ya walemavu ya Olimpiki ya Tokyo 2020. Kwa mujibu NPC ujumbe wa watu 18 wa timu ya wanawake ulifika Kigali septemba 18 na kama timu nyingine washiriki walipaswa kulipa $750 kabla ya kuingia kwenye hoteli ya Classic. Baada ya kuulizwa malipo walisema mtu mwenye pesa atawasili siku inayofuata hata hivyo mtu huyo hakutokea. Kisa hicho pia kimetokea kwa upande wa timu ya wanaume.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako