• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Mourinho ashika nafasi ya Pili duniani kwa makocha wanapokea Mkwanja mrefu zaidi

  (GMT+08:00) 2019-11-22 08:56:49

  Jose Mourinho amekuwa kocha wa pili duniani katika mchezo wa soka kulipwa fedha nyingi zaidi baada ya kuangusha saini ndani ya klabu ya Tottenham ambayo itakuwa inampatia kiasi cha pauni milioni 15 kwa mwaka kiasi ambacho kinamfanya kushika nafasi ya pili (2), kwa malipo ambayo wanalipa makocha wanaofundisha mchezo wa soka. Kusaini kwake tu, kwa miamba hiyo ya soka ya Kaskazini mwa jiji la London, Mourinho atakuwa anapokea kitita cha fedha mara mbili ya mshahara ambao alikuwa akilipwa kocha aliyetimuliwa kazi, Mauricio Pochettino. Hii ni kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu ya Tottenham, kumwajiri kocha ambaye tayari ameshinda mataji 25 kwenye taaluma hiyo huku wakitoa kitita kinono. Mreno huyo anakuwa nyuma ya Pep Guardiola ambaye anashika nafasi ya kwanza akipokea Pauni Milioni 20 baada ya kuongeza mkataba wake ndani ya Manchester City msimu uliyopita 2018 ambao atashuhudiwa akiwa hapo kwa miaka mingine miwili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako