• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • TENISI: Mkenya Okutoyi kucheza nusu fainali ya michuano ya ITF

  (GMT+08:00) 2019-11-22 08:57:07
  Mkenya Angela Okutoyi jana alijikatia tiketi ya kucheza nusu fainali katika mzunguko wa pili wa Mashindano ya Kimataifa ya Shirikisho la Tenisi kwa vijana wadogo ITF baada ya kumgaragaza mpinzani wake, Motisoa Rasendra wa Madagascar kwa 6-4, 6-0 katika Nairobi Club. Okutoyi mwenye miaka 15 ni mchezaji pekee wa Kenya aliyebaki katika mzunguko w apili wa mashindano ya wiki moja. Katika mzunguko wa kwanza wachezaji wenzake wa Kenya walitolewa kwenye hatua ya 16 bora iliyochezwa kati ya Jumatatu na Jumatano. Okutoyi alimuondoa Sabira Mohamed wa Marekani kwa 6-2, 7-5 siku ya Jumatano katika hatua ya 16 na kufanikiwa kuingia robo fainali.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako