• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini na Marekani wafanya mazungumzo kwa njia ya simu

    (GMT+08:00) 2019-11-22 16:50:52

    Waziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini Kang Kyung-wha na mwenzake wa Marekani Mike Pompeo wameongea kwa njia ya simu na kubadilishana maoni kuhusu masuala yanayofuatiliwa na pande hizo mbili, ikiwemo Makubaliano ya Jumla ya Taarifa za Kijeshi (GSOMIA) na kugharamia kwa pamoja kikosi cha Marekani nchini Korea Kusini(USFK).

    Mawaziri hao wamekubaliana kuendelea na mawasiliano ya karibu kuhusu masuala mbalimbali katika ngazi zote, na kuonyesha haja ya kukutana katika siku za karibuni ili kujadiliana kwa kina kuhusu masuala hayo.

    Mazungumzo hayo yamefanyika kabla ya kumalizika kwa Makubaliano hayo siku ya Jumamosi, ambayo yalisainiwa na Korea Kusini na Japan mwaka 2016, kubadilishana taarifa za kiintelijensia kuhusu mradi wa nyuklia wa Korea Kaskazini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako