Wakati akijua mpinzani wake kuelekea nusu fainali ya mashindano ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Challenge Cup) kwa Wanawake, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania Bara Kilimanjaro Queens Bw. Bakari Shime amesema mchezo wa mwisho dhidi ya Zanzibar Queens aliwapumzisha baadhi ya nyota wake kwa ajili ya hatua inayofuata. Baada ya kuichapa Uganda 3 – 0 katika mchezo uliochezwa jana, Kenya imechukua nafasi ya pili kwenye kundi B, na Kilimanjaro Queens itakutana na Waganda hao katika hatua ya nusu fainali.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |