• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda: Taakwimu zaonesha walioingia kwenye umaskini wameongezeka Uganda

  (GMT+08:00) 2019-11-22 18:27:09
  Uchunguzi wa Jopo la Kitaifa la Uganda unaonyesha kuwa asilimia 8.4, ambayo inawakilisha watu 338,520 wameingia kwenye umaskini katika mwaka wa fedha wa 2018/19.

  Matokeo yaliyotolewa na Ofisi ya Takwimu ya Uganda (Ubos) pia yanaonyesha kuwa asilimia 4.5 ya raia wa Uganda walioko mijini wamerejea kwenye umaskini ikilinganishwa na asilimia 10.4 katika maeneo ya vijijini.

  Hii kulingana na Ubos inahitaji uchambuzi zaidi ili kuelewa ni kwanini Waganda wengi wanarudi kwenye umasikini.

  Akiwasilisha matokeo hayo jijini Kampala, mwana takwimu wa ngazi ya juu Bwana Danstan Aguta, alisema kuwa kwa kiwango cha kitaifa asilimia 8.5. Kulingana na matokeo, Waganda hutumia asilimia 41.5 ya mapato yao kwa chakula, asilimia 3.7 kwa afya, asilimia 6.2 kwa usafirishaji, asilimia 19.4 kwa makazi, maji, gesi ya umeme, na mafuta na asilimia 2.5 hutumika kwa mavazi na viatu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako