• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Abiria watakiwa kupata risiti sehemu za vyakula

    (GMT+08:00) 2019-11-22 18:27:28
    Meneja wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Mkoa wa Kilimanjaro, Gabriel Mwangosi, amewataka abiria wote wanaosafiri kwenda mikoani, kudai risiti wanapofika katika maeneo ya kununua vyakula.

    Alisema abiria wengi hawana tabia ya kuchukua risiti wanapopewa huduma jambo ambalo ni kinyume na sheria na taratibu za nchi.

    Alisema baadhi ya maofisa wa TRA wako katika maeneo hayo kwa ajili ya ukaguzi wa matumizi sahihi ya mashine za kielektroniki za (EFD) na atakayekutwa na hatia adhabu ni faini ya kuanzia Sh. 30,000 mpaka Sh. 1,500,000 kwa mnunuzi asiyedai risiti ya huduma au bidhaa.

    Elias Sichuma, ni dereva wa mabasi makubwa anayefanya safari zake Moshi - Morogoro, alisema elimu kwa wamiliki wa maeneo ya vyakula na abiria inahitajika pamoja na madereva kuhakikisha wanatoa elimu kwa abiria kabla hawajashuka kupata huduma hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako