• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Rwanda kuwa mwenyeji wa mkutano wa chakula

    (GMT+08:00) 2019-11-22 18:27:52

    Rwanda, mwaka ujao itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Chakula wa Afrika, hafla ambayo inalenga kuweka mikakati ya kumaliza njaa na utapiamlo.

    Mwanzilishi na Mwenyekiti wa kampuni ya seeds and Chips Marco Gualtieri amesema Mkutano huo unawalenga zaidi ya washiriki 3,000 kutoka katika bara la Afrika na kote duniani, alisema.

    Amesema kukosekana kwa chakula, ni mojawepo wa changamoto kubwa zaidi kwa nchi zinazoendelea.

    Gualtieri alisema kuwa matumizi ya teknolojia yanaweza kuleta mabadiliko katika kuharakisha mchakato wa kuboresha mfumo wa chakula.

    Kulingana na shirika la Kilimo na Chakula duniani FAO karibu watu milioni 260 barani Afrika wanakabiliwa na njaa.

    Na ulimwenguni kote, kuna wastani wa watu milioni 820 wenye njaa - au karibu asilimia 11 ya idadi ya watu ulimwenguni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako