• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la uchumi wa uvumbuzi la mwaka 2019 latafuta ufumbuzi wa masuala ya uchumi duniani

    (GMT+08:00) 2019-11-22 18:33:31

    Baraza la uchumi wa uvumbuzi la mwaka 2019 limefunguliwa jana hapa Beijing, likiwa na kauli mbiu ya "uchumi mpya, mustakabali mpya". Baraza hilo limewashirikisha wajumbe 600 wakiwemo maofisa wa serikali, wanasiasa wastaafu, wanaviwanda na wasomi wa China na nchi za nje, ambao wamebadilishana maoni na kutafuta ufumbuzi wa masuala muhimu yanayoukabili uchumi wa dunia kwa hivi sasa.

    Mtendaji mkuu wa Kundi la UBS ambalo ni moja kati ya makampuni makubwa zaidi ya usimamizi wa mali duniani Bw. Sergio Ermotti amesifu sana pendekezo la China la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", akisema kuwa Uswis inafurahia pendekezo hilo litakaloiletea Ulaya faida kubwa katika sekta mbalimbali zikiwemo miundombinu na fedha.

    "Tunafurahishwa sana na Pendekezo la 'Ukanda Mmoja, Njia Moja', kwani Ulaya inahitaji sana miundombinu, na tumepata mabadiliko makubwa kupitia uwekezaji wa ujenzi huo."

    Ili kukabiliana na changamoto mpya zinazoukabili uchumi wa dunia, washiriki wengi wameeleza kuwa inahitajika kupanua ushirikiano na ufunguaji mlango. Mwanzilishi wa Kampuni ya Microsoft Bw. Bill Gates ameeleza kuwa, ushirikiano utaleta hadhi ya kuongoza, kinyume chake, kujilinda kutakwamisha maendeleo.

    "Maendeleo ya akili bandia ni mwelekeo usioweza kuzuilika. Ashikaye msimamo wa kufungua mlango, atapata hadhi ya kuongoza, kinyume chake, kujilinda kutakwamisha mchakato wa maendeleo. Unaweza kuwapuuza wale wasiopenda kufungua mlango kwa nje."

    Uhusiano kati ya China na Marekani ni suala lingine lililotajwa mara kwa mara kwenye baraza hilo. Aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Henry Kissinger ameeleza kuwa, umuhimu wa uhusiano kati ya China na Marekani, zikiwa kundi la pili na la kwanza la kiuchumi duniani, unakubaliwa na watu. Ana matumaini makubwa juu ya uhusiano kati ya pande hizo mbili katika siku za baadaye, na kusisitiza umuhimu wa mazungumzo kati ya pande hizo mbili.

    "Kwa kukabiliwa na hali mpya, uhusiano kati ya pande hizo mbili unapaswa kutatuliwa kwa njia ya kusaidiana. Natumai kuwa mazungumzo ya biashara kati ya pande hizo mbili yataweza kupata mafanikio, na kuwa mwanzo wa mazungumzo ya siasa yatakayofanyika katika siku za baadaye."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako