• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapongeza Russia kwa kuikosoa Marekani kuzuia maendeleo ya nchi hizo mbili

    (GMT+08:00) 2019-11-22 18:57:19

    China imempongeza rais Vladimir Putin wa Russia kwa kuikosoa Marekani kuzuia maendeleo ya China na Russia, na kusema nchi hizo mbili zina wajibu na majukumu ya kihistoria ya kulinda amani, utulivu, usawa na haki duniani.

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Geng Shuang amesema hayo alipoulizwa kuhusu kauli ya rais Putin katika kongamano moja la uwekezaji lililofanyika mjini Russia, akisema ni kosa kubwa kwa Marekani kukwamisha maendeleo ya China na Russia. Geng amesema kwa muda mrefu, Marekani imetetea sera ya upande mmoja, kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine, kutumia ovyo hatua ya vikwazo, na kuathiri vibaya utaratibu na kuharibu mifumo iliyopo ya kimataifa.

    Bw. Geng ameongeza kuwa, kwa kufuata makubaliano yaliyofikiwa na marais wa China na Russia, nchi hizo zitazidisha uaminifu wa kisiasa, kudumisha mawasiliano ya kimkakati, kupanua wigo wa ushirikiano, kuungana mkono zaidi na kukuza uhusiano wa wenzi wa uratibu wa kimkakati wa pande zote katika zama mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako