Waziri wa fedha wa China Bw. Liu Kun amesema, China itaongeza nguvu na kuchukua hatua zenye ufanisi zaidi ili kuboresha mazingira yake ya kibiashara.
Bw. Liu amesema China siku zote inafuatilia kiwango bora zaidi katika kuboresha mazingira yake ya kibiashara, kujifunza uzoefu wa kisasa wa kimataifa, kufuata kanuni za kimataifa na kuweka lengo la kufanya baadhi ya mageuzi yaongoze mwelekeo wa dunia. Pia inataka baadhi ya sekta kupiku zile za kiwango kizuri na sekta nyingine kuwa mbele, ili kuongeza zaidi nguvu ya ushindani wa biashara ya kimataifa, na kuchangia busara na mipango ya China kwa maboresho ya pamoja ya mazingira ya kibiashara duniani.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa hivi karibuni na Benki ya Dunia kuhusu mazingira ya kibiashara mwaka 2020, China ilipanda kwa nafasi 15 kuliko mwaka jana na kushika nafasi ya 31, ambayo ni bora zaidi kwa China tangu ripoti hiyo itolewe kwa mara ya kwanza.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |