• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Majaribio ya kuvuruga Hongkong kamwe hayatafanikiwa

    (GMT+08:00) 2019-11-22 19:25:52

    Hivi karibuni bunge la Marekani limepitisha Sheria kuhusu haki za kibinadamu na demokrasia ya Hongkong ya mwaka 2019, likiwaunga mkono wazi wazi waandamanaji wenye siasa kali wanaotumia mabavu, na kuingilia kati mambo ya ndani ya China, jambo ambalo lina nia mbaya na kwenda kinyume cha maoni ya raia, na madhumuni yake kamwe hayatafanikiwa.

    Lengo la kwanza la hatua hiyo ya Marekani ni kuchochea waandamanaji wenye siasa kali wanaotumia mabavu mkoani Hongkong ili kuwafanya waendelee kufanya vurugu. Pili, ni kutishia na kupambana na walinzi wa utulivu wa Hongkong, na kujaribu kuharibu sera ya "China moja, Mifumo miwili", na tatu, ni kukwamisha maendeleo ya China kwa njia ya kuingilia mambo ya Hongkong.

    Lakini ukweli ni kwamba, hadhi yenye umaalumu wa kipekee ya uchumi na biashara ya Hongkong inatokana na sheria za kimsingi, wala si faida zinazoletwa na Marekani. Maendeleo ya China, ustawi wa taifa, na ustawi wa watu vilevile zinatimizwa kutokana na juhudi zao zenyewe, si kutokana na faida zinazoletwa na Marekani.

    Nia imara ya serikali ya China ya kulinda mamlaka ya nchi, usalama na maslahi ya kujiendeleza kamwe haitabadilika, nia imara ya kutekeleza mwongozo wa "China moja, Mifumo miwili" kamwe haitabadilika, na nia imara ya kupambana na nguvu za nje za kuingilia mambo ya Hongkong kamwe haitabadilika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako