• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi asema, ndoto ya China haimaanishi kuwa juu ya mamlaka nyingine

  (GMT+08:00) 2019-11-22 19:47:08

  Rais Xi Jinping wa China amesema kuwa ndoto ya China, chachu kuu ya ufufuaji wa taifa la China, haimaanishi kuwa ni ndoto inayotaka kuwa juu ya mamlaka nyingine.

  Rais Xi amesema hayo alipokutana na wajumbe kutoka nchi za kigeni wanaohudhuria Kongamano la Uchumi wa Uvumbuzi la mwaka 2019 linalofanyika hapa Beijing. Amesema ana imani thabiti na hatma ya baadaye ya China, na kusema nchi hiyo haina lengo la kuchukua nafasi ya nchi nyingine, badala yake, inalenga kurejesha hadhi na nafasi inayostahili.

  Amesisitiza kuwa, historia ya kudhalilisha ya China kama nchi ya ukoloni na ubepari kamwe haitajirudia.

  Rais Xi ameongeza kuwa uvumbuzi ni kauli mbiu kuu ya zama za leo na hakuna nchi moja inayoweza kuwa kitovu cha uvumbuzi kinachojitegemea ama kunufaika na matokeo ya uvumbuzi peke yake. Amesema China na Marekani zote ni nchi kubwa za uvumbuzi, na China inapenda kushirikiana na nchi mbalimbali ikiwemo Marekani katika sekta ya uvumbuzi ili kunufaisha watu wa pande mbili na wa dunia nzima.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako