• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Novemba 16-Novemba 22)

  (GMT+08:00) 2019-11-22 21:11:20

  Sri Lanka yamuapisha rais mpya

  Rais mpya wa Sri Lanka Gotabaya Rajapaska ameapishwa kuwa rais Jumatatu.

  Vyanzo vya habari viliripoti kuwa hafla ya kuapishwa kwake ilifanyika kwenye hekalu la Kibudha la Runawell lililoko mji wa kaskazini.

  Rajapaska ameziomba jamii za walio wachache kutoka Tamil na Waislam ambao hawakumpigia kura kushirikiana naye katika kujenga taifa.

  Jamii zote mbili wakati wa kampeni zilieleza wasiwasi wao kutokana na ushindi wake kwa sababu ya msimamo wake mkali wa kijeshi wakati akiwa chini ya serikali ya kaka yake mkubwa, rais wa zamani Mahinda Rajapaska.

  Wakati wa kuapishwa kwake, rais huyo mpya ameahidi kuwa suala la usalama wa ndani litakuwa kipaumbele kwenye utawala wake.

  Sri Lanka ilikumbwa na mashambulizi ya kujitoa muhanga wakati wa sikukuu ya Pasaka ambapo watu 269 waliuawa.

  Kiongozi huyo mpya mwenye umri wa miaka 70 aliongoza operesheni ya kijeshi dhidi ya wapiganaji wa Tamil miaka 10 iliyopita. Rajapaska alimshinda mpinzani wake Sajith.


  1  2  3  4  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako