• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China asema China inajitahidi kuisaidia Afrika kuondokana na hali ya kutojiendeleza

    (GMT+08:00) 2019-11-23 17:02:33

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi leo amehudhuria mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za G20 huko Nagoya, Japan.

    Bw. Wang Yi amesema China inaunga mkono G20 kutoa msukumo wa kisiasa katika utekelezaji wa makubaliano ya Paris, na kushirikiana na pande mbalimbali kuhimiza mkutano wa 25 wa nchi zinazosaini mkataba wa mfumo wa mabadiliko ya hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa.

    Amesema, China inaunga mkono G20 kwa muda mrefu kuweka kipaumbele kwenye mada zinazohusu Afrika, kuisaidia Afrika kutatua masuala matatu ya kimaendeleo ambayo ni hali mbaya ya miundo mbinu, upungufu wa watu na ukosefu wa fedha, na kutatua masuala matatu ya kimaisha yakiwemo, ajira, chakula na afya, ili kuisaidia Afrika kujitoa kwenye hali ya kutojiendeleza.

    Amesema, ukosefu wa fedha ni changamoto kubwa inayozuia maendeleo ya Afrika, kila mwaka ukosefu wa uwekezaji katika ujenzi wa miundo mbinu umefikia dola za kimarekani bilioni 100. Na China imeisaidia Afrika kupata faida zaidi ya dola za kimarekani bilioni 50 katika ujenzi wa miundo mbinu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako