• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watanzania 1700 wanajifunza lugha ya Kichina

    (GMT+08:00) 2019-11-25 08:12:49

    VIJANA wa Tanzania 1700 wanajifunza lugha ya kichina nchini huku wachina 10 kila mwaka wakijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kusoma lugha ya Kiswahili.

    Sambamba na hilo vyuo vikuu vinne nchini China vikitoa shahada ya lugha ya kiswahili.

    Naibu waziri wa elimu, sayansi na teknolojia, William Ole Nasha amebainisha hayo wakati wa sherehe ya utoaji "Tuzo ya balozi wa China" nchini kwa wanafunzi 80 wanaosoma lugha ya kichina katika taasisi za Confucius zilizopo UDSM, Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) madarasa katika Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro pamoja na Sekondari 14.

    Akizungumza katika hafla hiyo, Ole Nasha alisema watanzania wanatakiwa kujifunza lugha ya kichina ili kukamata fursa za ajira, ufadhili katika Nyanja mbalimbali, teknolojia pamoja na kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo.

    Alisema kwa uhusiano uliopo baina ya China na Tanzania uliodumu kwa takribani miaka 50 ilitakiwa kila nchi kuongea lugha moja kwa watanzania kuzungumza Kichina na wachina kuzungumza Kiswahili.

    "marafiki wa kweli huwa wanaongea lugha moja, hivyo kwa sisi ilibidi kuwa tunaelewa tumechelewa lakini sasa ni wakati wa kutimiza hili" Alisema.

    Naibu waziri alisema nafasi ya China kiuchumi duniani hakuna awezaye kukwepa katika kuimarisha mahusiano hususan katika Sayansi na Teknolojia huku lugha ya kichin, kupata ufadhili wa kusoma fani mbalimbali pamoja na ajira kwa makampuni ya kichina yanayoongoza kwa uwekezaji Afrika.

    Akizungumza katika hafla hiyo,Balozi wa China nchini Tanzania ,Wang Ke alisema mwaka jana Ubalozi ulianza kutoa Tuzo ya Balozikwa wanafunzi wa Tanzania na mwaka huu wanafuzni 20 watapata tuzo bora na wengine 60 watapata tuzo ya mafanikio kutoka vyuo mbalimbali na shule ili kuhimiza vijana wengi kujifunza lugha hiyo.

    Pia kupata, ufadhili wa China kusoma nchini China hapo baadaye kwani mpaka sasa kuna taasisi mbili za Confucius katika UDSM na UDOM na kuna madarasa mawili katika Chuo kikuu Kiislamu cha na Habari cha Zanzibar.

    Ke alisema walimu 80 wa lugha ya Kichina wanafunzisha wanafunzi 1700 katika vyuo vikuu na chule mbalimbali nchini huku lugha ya Kiswahili imezingatiwa sna ana serikali ya China.

    "wachina wengi wa kampuni za China nchini wanafunza Kiswahili,ambacho kimesaidia kuleta uelewa na urafiki baina ya China na Tanzania "Alisema.

    Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi waliopata tuzo,mwanafunzi mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akizomea Shahada ya Elimu katika lugha ya Kiingereza na Kichina,Gloria Mshana alisema kujifunza lugha hiyo ni ngumu lakini kwa kuwa anaipenda anatumia muda mwingi kujifunza huku akisaidiwa na walimu wake.

    Alisema lengo la kujifunza lugha hiyo ni kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo ikiwemo kusaidia wananachi wake kuelewana kwa kuwatafsiria katika kampuni na shughuli mbalimbali huku akiwa na ndoto ya kufika China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako