• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TUZO: CAF yataja jumla ya wachezaji 30 watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka

    (GMT+08:00) 2019-11-25 08:41:50

    Shirikisho la soka barani Afrika CAF limetaja jumla ya wachezaji 30 ambao watawania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka ambapo miongoni mwao yumo mshambuliaji wa klabu ya KRC Genk na Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta. Kwa upande wa wachezaji ambao wanacheza ligi za ndani ya bara la Afrika yupo mshambuliaji wa klabu ya Simba, Meddie Kagere pamoja na Emmanuel Okwi ambaye msimu uliopita alipata mafanikio makubwa Simba ambaye kwa sasa anakipiga Itthad Alex SC. Nao Vipusa wa Harambee Starlets wameteuliwa kuwania tuzo ya timu bora ya wanawake mwaka huu ikiwa ni saa chache tu baada ya kuandikisha matokeo bora dhidi ya Burundi. Tuzo hizo ambazo hufanyika kila mwaka chini ya Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika CAF zinatarajiwa kutolewa Januari 7 mwaka 2020 Citadel Azure, Hurghada, nchini Misri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako